Please use this identifier to cite or link to this item:
http://localhost:80/jspui/handle/123456789/890
Title: | Mwongozo wa usimamizi na uvunaji endelevu wa mianzi aina ya simpodia. |
Other Titles: | ukilenga mianzi ya asili ya afrika |
Authors: | KEFRI |
Keywords: | Mianzi |
Issue Date: | 1-Jan-2020 |
Publisher: | INBAR |
Series/Report no.: | TAARIFA ZA KIUFUNDI Ethiopia Kenya Uganda; |
Abstract: | Mianzi ni aina ya nyasi. Kuna zaidi ya aina 1600 za mianzi ambazo zimeshambaa eneo pana katika maeneo ya hali ya hewa ya kitropiki na nusu tropiki Asia, Afrika na Amerika ya kusini. Ni mimea ya kudumu, inayokuwa kwa muda mfupi na ina nishati kubwa na ina uwezo wa kuzalisha vifaa/bidhaa zenye mchanganyiko ikiwa inatunzwa na kusimamiwa vizuri. Kuna matumizi zaidi ya 10,000 ya mianzi kuanzia matumizi ya bidhaa za chakula kama chakula cha binadamu, malisho ya wanyama na ndege (kuku) kutoka bidhaa ndogondogo mpaka bidhaa kubwa za viwandani. Uzalishaji wa bidhaa za mianzi kidunia na matumizi yake yanafikia thamani ya dola za kimarekani milioni 60 kukiwa na biashara ya bidhaa za mianzi zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 3 duniani. Hivyo, inatoa uwezo mkubwa kwa maendeleo ya kimaisha na uzalishaji wa kipato. Kwa kuongezea, mianzi inatupa faida kubwa za kimazingira zisizoonekana kama vile kuzuia mmomonyoko wa udongo, kuongeza ujazo wa maji katika chemichemi na makazi ya idadi ya wanyama wengi wa mwituni. Kwa kuzingatia taarifa ya tathmini iliyotolewa na FAO-INBAR (2007), kwa nchi sita za Afrika (Ethiopia, Kenya, Nigeria, Uganda, Tanzania na Zimbwabwe), zenye zaidi ya hekta milioni 2.7. Hivi karibuni, INBAR na Chuo kikuu cha Tsinghua, katika utafiti wa kuchunguza maeneo ya mbali yasiyofikika kirahisi kwa (2016) kwa nchi ya Ethiopia, Kenya na Uganda ilikadilia eneo ya uoto wa mianzi ni hekta milioni 1.66. Uchunguzi wa maeneo hayo, uliangalia ripoti ya tathmini ya rasilimali ya mianzi kwa nchi ya Madagaska na ikaonyesha maeneo yaliyo na uoto wa mianzi ni hekta zaidi ya milioni 1. Habari za idadi ya eneo la uoto wa rasilimali za mianzi kwa Afrika si kamili. Vilevile mianzi inapatikana kwa wingi kwa nchi za Tanzania, Nigeria, Msumbiji, Angola, Benini, Burundi, Camerooni, Jamhuri ya kati Afrika, Comoro, Ivory Coast, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Eritrea, Gabon, Gambia, Guine, Guine Bissau, Liberia, Malawi, Sierra Leone, Afrika ya kusini, Sudani, Togo na Zambia. Aina mbalimbali za mianzi iliyopo Afrika ni ndogo. Isipokuwa kwa nchi ya Madagasca ina aina nyingi za mianzi zaidi ya aina 30, nchi zingine Afrika zina aina chache za mianzi. Aina kuu mbili za mianzi asili inayopatikana sehemu kubwa ya bara la Afrika ni mianzi ya mwinuko - Oldeania alpina K. Schumach (sawa na Yushania alpina, Arundinaria alpina), kwa jina la kienyeji inaitwa mianzi ya sehemu za mwinuko, mara nyinyi inapatikana katika mwinuko wenye urefu wa mita 2300-4000 juu ya usawa wa bahari. Pia kuna aina mbili za mianzi iliyoletwa kutoka nje ya Afrika, kwa majina ni Bambusa vulgaris and Dendrocalamus giganteus imekuwa ni sawa na mianzi asili ambayo imekubaliana na mazingira ya Afrika na inapatikana sehemu nyingi za Afrika. Kwa kuongeza, zaidi ya aina 20 za mianzi zimeoteshwa Afrika na mashirika ya kitafiti na mashirika ya kimaendeleo zaidi kwa maeneo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika. |
Description: | A Swahili guideline on management and continuous harvesting of bamboo Simpodia |
URI: | http://localhost:8282/jspui/handle/123456789/890 |
Appears in Collections: | Guidelines/Extension Materials |
Files in This Item:
File | Description | Size | Format | |
---|---|---|---|---|
Swahili_Manual_Management of sympodial bamboo species.pdf | 12.1 MB | Adobe PDF | View/Open |
Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.